GOMA: Wakamatwa na polisi ya Congo, raiya wa nchi za kigeni wanao ishi kimagendo mjini humo
Alahamisi tarehe 23 mei 2024, meya wa mji wa GOMA mkokoani Kivu kaskazini, aliwaonyesha mbele vyombo vya habari , takrebani raiya kumi wa nchi za kigeni , wanao ishi mjini humo bila vitambulisho vya kuwaruhusu kuishi inchini DRC.
Kwa muujibu wa kamisa mkuu KAPEND KAMAND Faustin, kiongozi wa mji wa GOMA, watu Hao walikamatwa na vyombo vya usalama, usiku wa juma tano mei 22 mwaka wa 2024,wakati wa Doria waliyokuwa wakiendesha askari polisi na jeshi la Congo kwa pamoja, katika operesheni " Safisha mji wa GOMA" na ilikuwa ndani ya kata Lac Vert, Ndosho pia kata Kyeshero.
Walio kamatwa walikutwa na hatia ya kuishi kimagendo kwenye ardhi ya congo, na huwa wanasharikiana na adui wanao dhoofisha usalama wa raiya mjini Goma, kazi yao nikuwatolea taarifa kama wajasusi wa adui, Pia wana...