Butembo: msaada wa chakula kwa wa kimbizi wa vita wapelelwa sehemu isiyo fahamika
Chakula kilichoibwa na ambacho kilitolewa kwa Ajili ya wahamiaji wa vita pa Kanyabayonga tarafani lubero, mkoani kivu kaskazini,kimepatikana mjini Butembo kwa mama mfanyabiashara.
Idadi ya magunia ikiwa ni 877 ya unga wa mahindi yaliyokusudiwa kutolewa kwa familia waliokimbia makazi yao kwa sababu ya vita vya uvamizi vinavyo shuhudiwa tarafani Rutshuru, walio pata hifadhi mji mdogo wa Kanyabayonga, yalikamatwa na ngome ya kijeshi FARDC huko Butembo, pia kuwasilishwa kwa meya wa jiji hilo Alhamisi hii, Mei 30, 2024. Kwa mujibu wa mkaguzi wa hesabu za kijeshi, Meja GEORGES NKUWA, magunia hayo ya unga yalikamatwa kwa wasafirishaji baada yakuibwa kwenye gala za chakula cha watu waliohamishwa katika makaazi yao. "Hili tulilikamata kwenye malori yaliyokuwa yakiingia kusafirishwa kwenda sehemu...