Kuteuliuliwa kwa Wanawake watatu kama wamoja kati ya viongozi wa bunge la taifa la Congo, lililo simikwa rasmi hii juma tano tarehe 22 me 2024, ni dhahiri kwamba usawa wa kijinsia inchini DRC umeanja kuonekana.
Bi précieuse Petu afisa mkuu wa kitengo cha mawasiliano cha ofisi kuu ya kutetea haki haki za kijinsia, familia na watoto mkoani kivu kaskazini,alitoa maoni haya akizungumza na Beroyafm.net hii alahamisi tarehe 23 me 2p24. Huyo adhani kwamba, mfumo huo utabadili namna yakufanya kazi kwenye chumba cha bunge hilovhuko wakizingatia maslahi ya raiya wakati wakuchukuwa uamzi.
Tangu zamani, mwanamke haki yake imekanyagwa, na hii inafanya wasishiriki kwa uwingi maswala ya siasa. Kuchaguliwa kwa hao Wanawake,italeta nguvu mpya kwa nchi yao Congo kwa ujumla, na huenda ikawapa fursa wengine Wanawake kujitetea kwenye bunge bila hoga.
Bi précieuse Petu anaamini kwamba muda umefika, wakutetea maslahi ya jamii,hususan sana kutetea haki za mwanamke katika siasa za Congo.
Emmanuel kasereka toka Goma