RADIO BEROYA FM

dimanche, novembre 10News That Matters
Shadow

Beni: mauaji yana zidi sababu kubwa ndo hizo(nukuu ya mkaaji wa mahali)

Mauaji ya hivi karibuni ya rahiya wasio kuwa na hatia, yaliyo tekelezwa na magaidi wa ADF katika usultani wa baswagha madiwe tarafani Beni juma lilopita, na kusababisha raiya zaidi ya miya moja (100)kuyapoteza maisha yao,yamezungumziwa na wetu wengi.

Alipo zungumza na radio Beroya FM Goma hii juma tatu tarehe 10 juni 2024, raiya mmoja wa maeneo ambaye tumehifadhi jina lake kwa kumlindiya usalama ametaja sababu kubwa tatu zinazo sababisha kwa upande wake mauaji kudumu huko mda mrefu.

Kwanza : kupuuziya habari zinazo tolewa na raiya kwa wana jeshi wa FARDC wanaopatikana huko, hali hii ni moja wapo ya sababu kubwa zinazo changia kuuwawa kwa raiya na inamunufahisha adui kutekeleza mpango wake.

Pili: jambo lingine nikutowabadilisha wale askari jeshi ambao wamedumu mda mrefu huko « baadhi ya askari jeshi wamekuwa huko tangu mda mrefu,hii imepelekea wao kuwa hata na viwanja huko, wengine wanawafuga hata wanyama kama mbuzi,kuku,Pia wapo wanao tumiya hata magari ya kijeshi kwa shughuli za biashala kama kuuza miti,na mazao ya shamba, wanaweza kubadilishwa zaidi ya miya viongozi wa operesheni bila wale majeshi wa chini, usalama wa raiya utaendelea kuwa hatarini, tunaomba wabadilishwe pia wana jeshi wote sio tu viongozi wao>> amethibitisha raiya huyo.

Tatu: na la mwisho, kutokubali vijana wazalendo kupambana bega kwa bega na askari jeshi maeneo ya Beni,<< ukweli ni kwamba tumejiswali mengi , pale tunapo ona askari jeshi wanakataa kuwashirikisha vijana wetu katika kupambana na magaidi ADF,tuna jiuliza je sisi raiya wa beni tumetolewa kafara ao la ?

Kwa nini viongozi wasifanye kama walivyo fanya huko Rutshuru pia Masisi kuwaruhusu vijana wazalendo kupambana bega kwa bega na magaidi wa m23 iwe hivyo na kwetu Beni? » Kile tunacho kiomba ni kuwaruhusu vijana wazalendo kupambana pamoja na jeshi letu FARDC na wahasi wa ADF amesema kwa mwisho raiya huyo mkongomani.

Uhariri wa Beroya Fm Goma

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *