Chakula kilichoibwa na ambacho kilitolewa kwa Ajili ya wahamiaji wa vita pa Kanyabayonga tarafani lubero, mkoani kivu kaskazini,kimepatikana mjini Butembo kwa mama mfanyabiashara.
Idadi ya magunia ikiwa ni 877 ya unga wa mahindi yaliyokusudiwa kutolewa kwa familia waliokimbia makazi yao kwa sababu ya vita vya uvamizi vinavyo shuhudiwa tarafani Rutshuru, walio pata hifadhi mji mdogo wa Kanyabayonga, yalikamatwa na ngome ya kijeshi FARDC huko Butembo, pia kuwasilishwa kwa meya wa jiji hilo Alhamisi hii, Mei 30, 2024. Kwa mujibu wa mkaguzi wa hesabu za kijeshi, Meja GEORGES NKUWA, magunia hayo ya unga yalikamatwa kwa wasafirishaji baada yakuibwa kwenye gala za chakula cha watu waliohamishwa katika makaazi yao. « Hili tulilikamata kwenye malori yaliyokuwa yakiingia kusafirishwa kwenda sehemu nyingine kwa madhumuni ya kibiashara, tulikamata gunia takrebani 877 ,ambayo ndo kwanza tumeikabidhi kwa mkuu wamji wa Butembo kwa sababu pia kuna wakimbizi mjini naamini wanaweza kunufaika na hiyo, badala ya kuachwa mikononi mwa wananchi wasio waaminifu…, » alisema Meja GEORGES NKUWA. Kwa upande wake mkuu, wa mamlaka ya mji wa Butembo, kamishna mkuu MOWA BAEKI TELLY ROGER, alivipongeza vyombo vya usalama kwa kwa kazi walio ifanya ikiitaja kuwa ni nzuri pia alisisitiza kuwa wahalifu wote watakatishwa tamaa na adhabu za mfano zitatolewa dhidi yao.
watu waliokutwa na chakula hiki kiliyokusudiwa kwa wahanga wa vita, haswa wanawake walioandamana na mifuko hii ya unga kutoka Kanyabayonga hadi Beni wanasema kuwa walinunua vyakula hivi kutoka kwa wakimbizi waliopata bahati yakutolewa msaada Huo.
Nzangura Kwavingiston Negro