Secta yamlimo na ufugo mkoani Kivu kaskazini siku hizi imeonekana yenye kuasirika pa kubwa na vita, vinavyo shuhudiwa ndani ya Jimbo hilo, ambako vijiji kadhaa vimevamiwa na magaidi wa ADF, upande moja, upande mwingine na wanamgambo wa m23, na mengine makundi yenye kumiliki silaha kinyume na sheria, ambao wamesababisha raiya wengi kuyahama makaazi yao, kwenye vijiji ambako wengi walikuwa wakiendesha shughuli za mlimo na za ufugo, alibaini hayo Bwana Tembo Kasekwa Aniceth, mwenye kiti wa mlimo mkoani Kivu kaskazini.
Kiongozi huyu alipo zungumza na Beroyafm.net hii juma tatu 27 mei 2024,hapa mji mku wa Kivu kaskazini Goma, adokeza kwamba ukosefu wa usalama ni moja kati ya vyanzo vinavyo sababisha uhaba wa vyakula ndani ya jimbo hilo. Walimaji wengi wamelazimishwa kuondoka kwenye shamba zao wakihofia usalama wao, alitujuza Tembo Kasekwa. Upande mwingine ameonyesha kinaga ubaga kwamba ardhi ya congo, hususani sana mkoani kivu kaskazini, udogo unatoa mazao ya shamba kwa kila mmeya, na raiya wakipata amani, wako tayari kuwalisha familia zao kupitia mazao ya shamba, pia kulisha nchi kwa ujumla isitoshe, kwa nini wasilishe mataifa mengine? Adhani hivyo kiongozi huyo.
Hatimaye amesema kwamba anaamini raisi wa DRC kwa jitihada anazo zifanya, ili kurejesha amani mashariki mwa DRC.
Emmanuel kasereka kutoka Goma