RADIO BEROYA FM

dimanche, janvier 18News That Matters
Shadow

RDC: Mchambuzi wa kisiasa John Awaze azungumzia jaribio ya mapinduzi didjini Kinshasa

Akitoa maoni yake kuhusu yaliyo tukia Kinshasa Gombe, juma pili tarehe 19 mei 2024,John Awaze, mchambuzi wa siasa za Congo DRC anaye jitegemea, anaye ishi mjini Goma mashariki mwa DRC , ataja jaribio hili kama ukosefu wa akili kwa wahusika,lililo ongozwa naye Christian Malanga na kundi lake.

Akijadiliana na radio Beroya FM GOMA, mchambuzi huyo, adhani kwamba viongozi wa serekali ya Congo, wanayo jukumu kubwa Siku hizi,na mojawapo ya Yale wanayo takiwa kufanya, ni kuleta Amani mashariki mwa nchi hiyo, ikiwa ndo haja ya kila mkongomani mwenye kuipenda inchi yake,

Huyo hajaona upande wake umuhimu wa watu wanao jidai kuwa wa kongomani wajitokeze na kuleta vurugu, jambo hili ni lakupiga marufuku.
Congo inahitaji mambo mengine sio upuuzi walio ufanya Christian Malanga na kundi lake eti kama wao wanaleta Zaïre mpya ni mambo ya ulimbukeni na ujinga tu ametangaza John Awaze.Mambo ya kuchukua madaraka ya inchi kimabavu upande wake mchambuzi wasiasa huyo, yamepitwa na wakati.

Kama kuna wakongomani walio na haja ya kuhudumu kwenye serekali, katiba ya Congo imeweka taratibu kuhusu jambo hili , wakongomani wanatakiwa kuipenda inchi yao na wawe wazalendo wa kweli, adhani mchambuzi huyo.

Emmanuel kasereka/Goma DRC.

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *