RADIO BEROYA FM

mardi, mars 10News That Matters
Shadow

Kinshasa : Kifo cha mwana mdogo wa Patrice Emery Lumumba, akiwa na umri wa miaka 68

Roland-Gilbert Okito Lumumba, mwana mdogo wa Patrice Emery Lumumba, Waziri Mkuu wa kwanza wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo chini ya Joseph Kasavubu, ameaga dunia. Alizaliwa mwaka 1958, na kadhaa ya watu wa karibu na marehemu wanasema kwamba aliendeleza urithi wa kifamilia uliojaa alama ya historia ya kisiasa ya taifa hilo.

Roland-Gilbert Okito Lumumba alifariki Jumatano tarehe 28 Januari 2026 mjini Kinshasa, mji mkuu wa kisiasa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ingawa aliishi mbali na misukosuko ya vyombo vya habari, jina lake liliendelea kuhusishwa na kumbukumbu ya baba yake, shujaa wa taifa na alama ya mapambano ya uhuru.

Kifo chake kinakumbusha uzito wa historia na mwendelezo wa urithi unaoendelea kuishi katika dhamira ya pamoja ya wananchi wa Kongo. Kwa kumbukumbu, baba yake mzazi pia aliuwawa katika jimbo la Katanga lililoongozwa na msaliti Moïse Tshombe, mnamo tarehe 17 Januari 1961, kwa baraka ya Ubelgiji.

            Kaseso Muhayirwa Elias

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *