RADIO BEROYA FM

lundi, mars 16News That Matters
Shadow

GAVI Yazindua Kampeni ya Kihistoria ya Chanjo kwa Watoto Milioni 62 Nchini DRC

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inajiandaa kupokea kampeni kubwa zaidi ya chanjo dhidi ya surua na rubela kuwahi kuandaliwa na Muungano wa Kimataifa wa Chanjo (GAVI), ikilenga kuwalinda watoto milioni 62.  

Rais wa Jamhuri, Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo, alipokea Jumanne tarehe 25 Novemba, katika Cité de l’Union Africaine, ujumbe wa GAVI ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Dkt. Sania Nishtar.

Katika mazungumzo hayo, Dkt. Nishtar alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya DRC na GAVI, akibainisha kuwa nchi hiyo ni miongoni mwa miradi mikubwa zaidi ya shirika hilo, ikiwa na uwekezaji wa jumla wa dola bilioni 2.2 za Kimarekani.

Aidha, alitangaza uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya chanjo dhidi ya surua na rubela, itakayofanyika kuanzia tarehe 27 Novemba hadi 1 Desemba 2025. Hii ni operesheni ya kiafya yenye upeo mpana zaidi kuwahi kutekelezwa na GAVI nchini DRC, ikiwalenga watoto wenye umri wa kuanzia miezi 9 hadi miaka 14.

Awamu ya kwanza ya kampeni itahusisha majimbo ya Grand Katanga, Bas-Uele, Haut-Uele na Ituri, kabla ya kuenea taratibu katika maeneo mengine ya taifa.

Mpango huu unakusudia kuimarisha ulinzi wa watoto wa Kongo dhidi ya magonjwa haya mawili yenye kuambukiza kwa kasi, katika mazingira ambapo DRC bado ni miongoni mwa nchi zilizo hatarini zaidi kukumbwa na milipuko ya surua.

Emmanuel Kasereka bin Vikingi

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *