RADIO BEROYA FM

mardi, août 11News That Matters
Shadow

Ebola Ituri: Uangalizi wa kitabibu waimarishwa huku mashirika ya kibinadamu yakirejea, asasi za kiraia zapongeza hatua hiyo

Katika eneo la afya la Aru, mkoani Ituri, zaidi ya watu 221 walionesha dalili zinazohusishwa na ugonjwa wa virusi vya Ebola kati ya mwezi Juni na Julai. Miongoni mwao, visa 25 vilithibitishwa kuwa na maambukizi ya Ebola, huku watu sita wakifariki dunia. Wagonjwa wanne wamepona, wakati wengine wanaendelea kupatiwa matibabu katika Kituo cha Tiba ya Ebola chini ya uangalizi wa wahudumu wa afya.

Mganga Mkuu wa Eneo la Afya la Aru, Dkt. Amanga Ama Jacques, amesisitiza kuwa dalili kama homa, kuhara, kutapika au kutokwa damu hazimaanishi moja kwa moja kuwa mtu ameambukizwa Ebola. Amewataka wananchi kufika mapema katika vituo vya afya kwa uchunguzi na matibabu, akieleza kuwa licha ya vifo vilivyoripotiwa, hali inaendelea kudhibitiwa.

Nyakunde: Mashirika ya kibinadamu yarejea

Wakati huo huo, asasi za kiraia za Ituri zimepongeza kurejea kwa mashirika ya kibinadamu katika eneo la afya la Nyakunde. Mashirika hayo yalikuwa yamesitisha shughuli zake kufuatia kuuawa kwa mfanyakazi mmoja wa kibinadamu tarehe 15 Julai mwaka huu.

Mratibu wa asasi hizo katika ngazi ya mkoa, Mhandisi Dieudonné Lossa, amesema kurejea kwa washirika hao kutaimarisha juhudi za kukabiliana na mlipuko wa Ebola. Pia amezitaka jamii za wenyeji kuunga mkono juhudi za serikali pamoja na washirika wake ili kudhibiti na hatimaye kumaliza maambukizi ya ugonjwa huo.

Na Daniel Ashuza

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *