RADIO BEROYA FM

mercredi, avril 15News That Matters
Shadow

CFO : Timu tatu za kwanza kufuzu nusu fainali za mashindano ya ndani zasikika

Mechi za kwanza za marudiano za mashindano ya ndani yanayoandaliwa na Cercle de Football d’Oicha (CFO) zilichezwa Jumapili tarehe 15 Machi katika viwanja mbalimbali vya eneo la Beni. Mwishoni mwa michezo hiyo, vilabu vitatu tayari vimehakikisha nafasi zao katika hatua ya nusu fainali ya mashindano haya.

Huko Oicha, FC Chui iliibuka na ushindi wa mabao 2–0 dhidi ya AS Miracle, na hivyo kuthibitisha tiketi yake ya kuingia katika nne bora.

Katika uwanja wa Mangina, TS Aigle Jaune pia ilihakikisha kufuzu baada ya ushindi mwembamba wa bao 1–0 dhidi ya AS Pointe Noire.

Nao huko Kasindi, pambano kati ya FC Volcan na FC Kasindi Sport liliisha kwa sare tasa ya 0–0 katika muda wa kawaida. Hatua ya mikwaju ya penalti ndiyo iliyetoa mshindi, ambapo FC Kasindi Sport ilionyesha ufanisi kwa kushinda kwa mikwaju 4–2.

Kwa matokeo haya, FC Chui, TS Aigle Jaune na FC Kasindi Sport ndizo timu tatu za kwanza kufuzu nusu fainali za mashindano ya ndani ya CFO.

Nafasi ya mwisho ya kufuzu itabaki kuamuliwa katika mechi mbili kati ya FC Kitenge Lac na CS Delta Force, ambazo ratiba yake tayari imetolewa na uongozi wa CFO.

 Benedicto Kaluba

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *