Kasese yawakaribisha mahujaji wa Kongo katika safari ya Namugongo
Jimbo Katoliki la Kasese, nchini Uganda, limefungua milango yake Ijumaa tarehe 15 Mei 2026 kwa kundi la kwanza la mahujaji wa Kikatoliki kutoka jimbo la Butembo-Beni, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Tukio hili limekuwa hatua muhimu katika hija ya miguu kuelekea kwenye madhabahu ya mashahidi wa Namugongo, alama ya imani na umoja wa Afrika Mashariki.
Kwa mara ya kwanza, jimbo la Kasese limepokea kundi la mahujaji 78 kutoka Butembo-Beni waliovuka mpaka kupitia daraja la Lhubiriha baada ya kulala usiku katika eneo la Lubiriha, parokia ya Mtakatifu Conrad wa Kasindi.
Mapema alfajiri, mahujaji walikamilisha taratibu za uhamiaji kabla ya kupokelewa na Mhashamu Francis Aquirinus Kibira, Askofu wa Kasese. Askofu aliongozana na ujumbe wa serikali kuu ya Uganda pamoja na viongozi wa eneo, ish...








