Beni: Ir Agronome Bienfait Kahehero akumbwa na wizi wa kutumia silaha, usalama wahitajika
Huko Beni, makao makuu ya muda ya mkoa wa Kivu Kaskazini, nyumba ya Ir agronome Bienfait Kahehero iliyoko katika commune Bungulu, mtaa wa Kanzulinzuli, seli ya Kahodokyo, barabara ya Kinyambili, imevamiwa na wahalifu waliokuwa na silaha.
Matukio haya ya uvunjaji wa sheria yalifanyika usiku wa kuamkia Jumatano tarehe 28 Januari 2026, kati ya saa 9 usiku na saa 10 alfajiri, kulingana na maelezo ya mhanga ambaye anasema aliokoka kwa miujiza.
Ir Bienfait Kahehero anaongeza kuwa wahalifu hao, waliokuwa jumla ya watu sita, walizingira makazi yake na kuvunja mlango wa kuingilia kwa kutumia kifaa cha mbao kinachojulikana kwa jina la Kasuku, kisha wakaingia ndani ya nyumba.
“Wahalifu wawili waliingia ndani ya nyumba, mmoja akiwa na bunduki tayari kwa matumizi, huku wanne wengine wakibaki nje w...




