RADIO BEROYA FM

mercredi, février 11News That Matters
Shadow

Beni michezo:Feu Rouge Yazimwa, Chui Yaibuka Mutwanga

Mashabiki wa Mutwanga wameshuhudia mwanzo wa moto: Chui wa Nzenga wakazima Feu Rouge kwa mabao matatu, huku Soins Système wakitibu Ruwenzori kwa bao moja pekee, na hamasa ikielekezwa kwa michezo ya leo Jumatatu.  

Katika Uwanja wa Mutwanga, hatua ya Inter-groupement ya Mashindano ya Soka ya Kijamii yaliyoandaliwa na Cercle de Football ya Oïcha ilianza rasmi Jumapili tarehe 04 Januari 2026, katika Uwanja wa 20 Mai.

Saa saba mchana (13h), FC Feu Rouge ya Bulongo ilipoteza mbele ya FC Chui ya Nzenga kwa mabao 3–1. Ushindi huu ulitokana na mabao mawili ya Patrick Mutalinge na bao moja la Kambale Basumbe maarufu Isco. Kikosi cha kocha Toto Manopi kilionekana makini na chenye maamuzi thabiti katika dakika zote za mchezo.

Bao la kwanza lilipatikana dakika ya 29 kupitia penalti iliyowekwa kimiani na Patrick Mutalinge, ambaye aliongeza bao la pili dakika ya 39. Hatua ya mwisho ya kuzima matumaini ya wapinzani ilikuja dakika ya 81, pale Kambale Basumbe Isco alipofunga bao la tatu, na kuhitimisha matokeo ya mabao 3–1 hadi mwisho wa muda wa kawaida.

Katika pambano la pili, AS Ruwenzori ya Mutwanga ilisalimu amri mbele ya Soins Système ya Bulongo kwa bao 1–0. Bao pekee na la ushindi lilifungwa dakika ya 57 na Kathembo Mupeleka Jadot, na kuandika historia ya mchezo huo.

Kwa Jumatatu tarehe 05 Januari 2026, ratiba ya siku ya pili ya mashindano haya inabashiri michezo mingine miwili:

 Saa saba mchana (13h), FC Kasindi Sport itakuwa mwenyeji wa Lume Sport.

Saa tisa alasiri (15h), AS Sukisa ya Lume itapokea AS Lubiriha Sport.

 Romulus Nzalumbo

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *